Jumamosi, 7 Februari 2015

andrew ayue alieipeleka ghana final

hizi ndizo mechi za ligi kuu ya soka ya tz bara wiki hii

TAREHE 7.2.2015

 16:00 POLISI MORO - : - AZAM FC

16:00 NDANDA FC - : - STAND UNITED

16:00 KAGERA SUGAR - : - MGAMBO JKT

16:00 T.PRISONS - : - RUVU SHOOTING
 16:00 JKT RUVU- : - MBEYA CITY

16:00 COASTAL UNION - : - SIMBA SC


 MICHEZO INAYOKUJA

 2015-02-08 16:00 YANGA Vs MTIBWA SUGAR Uwanja wa taifa

RnTimuPWDLFAGdPts
1YANGA12642137622
2Azam FC11632158721
3MTIBWA SUGAR11461137618
4POLISI MORO13463109118
5JKT RUVU135351313018
6RUVU SHOOTING1353599018
7Coastal Union13454109117
8SIMBA SC123721311216
9MBEYA CITY1243588015
10KAGERA SUGAR133641011-115
11MGAMBO SHOOTING11425610-414
12NDANDA FC134271117-614
13STAND UNITED13256816-811
14T. PRISONS12174911-210

MASHART YA KOPUNOVIC KWA BEKI OWINO


Kocha wa Simba, Goran Kopunovic, amempa masharti magumu beki wa timu yake hiyo, Joseph Owino ambaye amerejea uwanjani hivi karibuni baada ya kukaa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama paja.

Owino alianza mazoezi mepesi wiki iliyopita na anatarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake hivi karibuni, hivyo akirudi kikosini kutakuwa na vita kubwa ya namba kati yake na mabeki Hassan Isihaka na Juuko Murshid ambao kwa sasa wapo kwenye kiwango kizuri.
Kopunovic amesema hawezi kumpa nafasi kwa kuwa anahitaji kuangalia kiwango chake na nidhamu kabla ya kumpa nafasi ya kucheza licha ya kuwa Owino alikuwa nahodha wa timu hiyo kabla kocha huyo hajatua klabuni hapo.
“Owino ana nafasi ya kucheza japo mabeki wote wapo katika viwango vizuri, lakini siwezi kusema namhakikishia namba kwa sasa, lazima aonyeshe kiwango.
“Sipendi kumuona beki ambaye katika kila mchezo anapewa kadi au kusababisha penalti, kama hatakuwa na tabia hizo basi ana nafasi kubwa ya kucheza,” alisema Kopunovic.

ILE ISHU YA BUSU KANAVARIO AMUOMBA MSAMAHA YULE ASKARI WA KIKE



Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amemuomba radhi askari aliyemkimbilia na kwenda kumkumbatia dakika chache baada ya kufunga bao katika mechi dhidi ya Coastal Union.

Cannavaro alifunga bao hilo katika dakika ya 11, Jumatano iliyopita na kufanya kitendo hicho ambacho kilikuwa gumzo.
 Cannavaro alisema alimuomba askari huyo msamaha muda mfupi baada ya mechi hiyo ambapo aliamua kumfuata na kumueleza kuwa hakuwa na nia mbaya.
Cannavaro alisema anamshukuru askari huyo kwa kukubali maombi yake ya msamaha aliyoyatoa kwani hakutarajia hali hiyo kutokea kutokana na furaha aliyoipata baada ya kufunga bao hilo.
“Kiukweli nilifanya kosa kukimbia na kwenda kumkumbatia askari wakati nashangilia bao nililolifunga, nilijikuta ghafla nafanya kitendo kile bila kutarajia, sikukitarajia kabisa wala sikupanga iwe hivyo.

“Baada ya mechi kumalizika nilimfuata nikazungumza naye, pia walikuwepo baadhi ya viongozi wangu na wale wa polisi niliwaomba radhi kwa kitendo hicho nilichokifanya, 
nikashukuru wakanielewa na kulimaliza tatizo hilo,” alisema Cannav


TABIA za beki mkongwe wa Chelsea, John Terry, ni kupenda kujitambulisha kwa washambuliaji anaokutana nao wakati timu yake ikiwa uwanjani.
Terry, maarufu kama JT, hajitambulishi kwa kupeana mikono, badala yake maneno ya kibabe au kumgongagonga mshambuliaji anayekuwa anamkaba ili kumuonyesha siku hiyo shughuli ni pevu.

Nahodha huyo wa Chelsea amekuwa akifanya hivyo mara nyingi ikionekana kutaka kumtawala mapema kabisa kisaikolojia mshambuliaji anayemkaba kwamba ajue amekutana na kiboko yake au beki katili na asiyetaka mchezo na kazi yake.
Wakati akiwa Liverpool, mshambuliaji Fernando Torres aliwahi kusema kila walipokutana na Chelsea alifanya juhudi kubwa kuhakikisha anafunga kwa kuwa alitaka kumuonyesha Terry ambaye hakufurahishwa na ubabe wake mara kwa mara.
Huenda mara kadhaa, Terry amekuwa akibadili mbinu zake, lakini hiyo ni moja ya kubwa alizonazo. Wakati fulani, mpango huo wa Terry ulifeli.

Katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, Terry alianza mapema mipango yake ya kutaka kumuonyesha mshambuliaji Diego Costa kwamba yeye ni nani. 
 
Lakini majibu yalikuwa makali kuliko alivyotegemea na ndipo akagundua kuwa Costa ni namba nyingine na huenda mfumo alioutumia kwa mara ya kwanza haukuwa sahihi.
Kitendo cha Costa kuwakanyaga mabeki Emre Can na Martin Skrtel wa Liverpool kimewafanya wengi waamshe mjadala wa mshambuliaji huyo raia wa Hispania mwenye asili ya Brazil.
Maswali yamekuwa ni mengi, kama kweli anafaa kuichezea Chelsea, kama kweli wanastahili kuwa na mchezaji mkatili hivyo. Mwisho wengi wanahoji vipi awe mjeuri namna hiyo? Ingawa wanavutiwa na uwezo wa kazi zake maana ndiye anaongozwa kwa kutikisa nyavu katika Ligi Kuu England.
Costa ni mtoto wa Uswahilini, amekulia maisha hayo na hakuwahi kuishi maisha ya mafunzo ya soccer kwenye ‘academy’ kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Ulaya.
Ubabe wa mechi za mchangani ambazo alikuwa maarufu sana, bado uko kwenye damu yake, ndiyo maana anawapa tabu sana Wazungu.
Costa alizaliwa katika mji mdogo wa Lagarto katika Jimbo la Sergipe nchini Brazil. Miaka yote alikuwa akicheza soka la mchangani na alikuwa maarufu sana.
Hadi alipofikisha miaka 16, ndiyo alichukuliwa hadi jijini Sao Paulo na kujiunga na timu iliyokuwa na mafunzo sahihi ya mchezo wa soka.
 
Waliocheza naye soka katika Mji wa Lagarto kabla hajaondoka kwenda Sao Paulo, wanasema alikuwa mjeuri, mtu mwenye hasira na hakuwa na woga hata kidogo.
Lakini kituko cha kumpiga mchezaji halafu akakimbilia kumsukuma na kumghasi mwamuzi kilikuwa maarufu zaidi. Baadaye Costa alifungiwa miezi minne. Wakati huo alikuwa akiichezea Barcelona Esportiva Capella.
Aliwahi kubatizwa jina la Picardia, neno hilo la Kihispania lenye maana ya mpiganaji au mtu asiye na hofu na ndivyo anavyoonekana.
Hii inaonyesha kiasi gani uchezaji wa kibabe Costa hautakwisha na ataendelea kuwa namna hiyo kwa kuwa hakucheza soka la mafunzo linalomuonyesha afanye vipi kuonekana ni mwenye nidhamu.
Takwimu zinaonyesha hata kabla ya msimu kwisha, ameshasababisha tafrani za kawaida mara 22, amekwidana na mabeki mara tano, amewasukuma kwa kifua mara 13, amewasukuma kwa mikono mara 15 na amekutana na mabeki uso kwa uso na kutoa maneno ya kibabe mara 11.
Pamoja na kwamba ameshakutana na adhabu kutoka FA, lakini haimbadilishi yeye kuwa alivyo na wengi wamekuwa wakisema ni zawadi nzuri kwa mabeki wa England ambao wengi wamekuwa wababe kwa washambuliaji.
 Mara kadhaa, Costa ameonekana akiwa amechaniwa jezi au bukta. Lakini amekuwa akionyesha sehemu alizoumizwa na viatu vyenye njumu za chuma za mabeki hao ambao sasa wameanza kulalamika.
Hakuna ubishi tena unaweza kusema ubabe wa Costa ni dawa ya mabeki wababe wa England na karibu kila mchezo amekuwa akizozana nao na mara nyingi kuwafanya wadau wa soka kuwaonea huruma mabeki.
 
Kwa zaidi ya miaka 20, hakuna aliyewahi kulalamika mabeki wa Ligi Kuu England wamekuwa wakionewa hadi Costa alipotua England. Je, ataendelea hivyo hadi mwisho?
Mabao anayofunga anaonyesha ana uwezo na hilo alilidhihirisha Hispania kabla ya kutua England. Je, kuna mengi anafunga baada ya kuwatisha mabeki?
 
Jiulize, mabeki wa England hasa wale wa kati ambao wengi ni wakatili, wataendelea kumvumilia na kushitaki bila ya kumtafutia dawa?
Ila ukweli, mtoto wa Uswahilini anawapa shughuli mabeki hao licha ya wao kutamba kwamba England ndiyo kwa wababe.
Kwa sasa Costa ni kati ya burudani zinazovutia zaidi katika soka England. Kila anapokuwa anaitumikia Chelsea, wengi hupenda kuona anavyofunga na sasa imegeuka, wengi wanapenda kuona anavyopambana na mabeki wababe.

07 Feb 2015


Kiungo Mkenya, Paul Raphael Kiongera ametishia kujiondoa mikononi mwa klabu ya Simba kama hakutakuwa na mabadiliko.

Kiongera ameliambia gazeti hili kuwa amechoshwa na kile alichokiita ‘uswahili mwingi’ ambapo anadai kutolipwa fedha yoyote tangu Desemba, mwaka jana.
Simba iliondoa jina la mchezaji huyo katika usajili wake wa msimu huu licha ya kuwa na mkataba naye, ambapo ilisema itaendelea kumlipa kama kawaida kwa kuwa itamhitaji baada ya kupona jeraha la goti lililokuwa likimsumbua na kusababisha akatibiwe nchini India ambapo Simba ndiyo iliyogharamia huduma zake.
Akizungumza kutoka jijini Nairobi, Kiongera amesema: 

 “Ni kweli nasubiri Februari hii iishe, nimalizane nao kwa kuwa kwa mujibu wa mkataba wetu, wao ndiyo watakuwa wamekiuka masharti na wameuvunja.
“Naona Simba wananizingua tu. Ujue hawataki kunipa mshahara wangu.”
Lakini Simba imesisitiza kwamba inamlipa fedha zake na hadai chochote.

Mwenyekiti wa Usajili, Zacharia Hans Poppe, alisema: “Kweli Kiongera tuna dhamana ya kumlipa na binafsi najua analipwa fedha zake na hakuna madai yoyote juu yetu. Sina taarifa zozote juu ya yeye kutolipwa kwa kuwa mi najua analipwa kama kawaida, vinginevyo aulizwe katibu.”

MSUVA,LUHENDE KILA MMOJA AJIGAMBA DHIDI YA MWENZAKE

Ongeza kichwa

Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva na beki wa pembeni wa Mtibwa Sugar, David Luhende, kila mmoja kwa muda wake ametoa vitisho vya kuhakikisha anamzimisha mwenzake katika mechi baina ya timu hizo kwenye Ligi Kuu Bara, kesho Jumapili.

Yanga inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mtibwa kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo Msuva ndiye amekuwa staa wa Yanga katika siku za hivi karibuni huku Luhende ndiye beki wa Mtibwa ambaye anaweza kukutana naye mara kwa mara ikiwa wote watacheza mechi hiyo.
Msuva ameliambia gazeti hili kuwa, yupo fiti kupambana na beki yeyote atakayekutana naye bila kujali ni Luhende au mwingine.
“Nikwambie ukweli tu, mimi nikiamua jambo langu uwanjani, hakuna mchezaji yeyote atakayenizuia, hivyo huyo beki wa Mtibwa atakayepangwa basi anatakiwa ajiandae.
“Kama atapangwa kuanza Luhende, itakuwa vizuri kwangu kwa sababu ninamjua vizuri, nitamtia hasira tu kwa kumpiga chenga za maudhi na kukokota mpira kwa kasi kwa ajili ya kumchosha,” alisema Msuva.
Upande wa Luhende ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga, alisema: “Mimi hakuna mshambuliaji ninayemhofia, nimejiandaa vizuri na mechi hiyo dhidi ya Yanga, sitaki kuongea sana, tuonane uwanjani.”

 

LEO NI SIKU YA DERBY KATIKA MAJIJI YA LIVERPOOL NA LONDON


LONDON, England
UTAMU wa soka la Ulaya utaendelea wikiendi hii. Vita ya kusaka ubingwa wa England nayo itazidi kupamba moto katika mechi za leo na kesho, lakini kubwa zaidi linalozungumzwa kitaa ni ‘derby’ (mechi zinazohusisha timu zinazotoka mji mmoja) mbili kubwa nchini England.

Derby ya kwanza inatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa White Hart Lane ambayo itazikutanisha timu zinazotokea katika Jiji la London, yaani Tottenham Hotspur dhidi ya Arsenal katika mtanange wa kukata na shoka utakaochezwa kuanzia saa 9:45 alasiri.
Lakini baadaye saa 2:30 usiku, kutakuwa na derby nyingine itakayozikutanisha timu zinazotokea jijini Liverpool, yaani Everton na Liverpool FC ambazo zitapambana vikali kwenye Uwanja wa Goodison Park.
Tottenham vs Arsenal
Vita hii inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka sehemu mbalimbali duniani. Mechi itachezeshwa na mwamuzi mkongwe, Martin Atkinson, raia wa England.
Utamu wa mechi hii unatokana na timu zote kuwa kwenye kiwango bora katika mechi zake za hivi karibuni. Katika michezo yao mitano iliyopita, Tottenham wameshinda mitatu, wametoa sare mmoja na kupoteza mmoja, wakati Arsenal wenyewe wameshinda michezo yao yote mitano iliyopita.
Katika michezo yao mitano iliyopita waliyokutana, Arsenal imeshinda mara tatu, wakati Spurs imeshinda mara moja tu huku zikitoka sare mara moja.
Hata hivyo, pamoja na Arsenal kushinda mara nyingi dhidi ya wapinzani wao hao katika siku za hivi karibuni, bado mpambano unatarajiwa kutotabirika kutokana na kiwango cha sasa cha Spurs ambayo inawategemea zaidi washambuliaji wake Harry Kane na Christian Eriksen walio kwenye ‘fomu’ kwa sasa.
Supastaa wa Arsenal, Mchile, Alexis Sanchez, anatarajiwa kuukosa mchezo huo wa leo kutokana na kuendelea kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja yaliyomuweka nje ya uwanja katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Aston Villa wiki iliyopita, lakini kocha Arsene Wenger atashusha pumzi kufuatia kurejea kwa mpachika mabao wake, Danny Welbeck.
Timu zote hizi, zipo katika mapambano ya kuhakikisha zinakuwemo ndani ya nne bora ili zipate nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Kama Arsenal iliyo katika nafasi ya tano ikishinda kwenye mtanange huu, itakuwa imeingia hadi kwenye mbio za kuwania ubingwa wa England kwa kuwa itakuwa imebakiza pointi nane tu iwafikie vinara Chelsea ambao baadaye watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Aston Villa. Lakini Spurs ikifungwa itakuwa inazidi kujiweka pabaya katika vita ya kuingia ‘top 4’.
Kama Spurs iliyo katika nafasi ya sita ikishinda mchezo huo, itaipiku Arsenal kwenye nafasi ya tano na inaweza ikaingia moja kwa moja ndani ya nne bora na kusubiri matokeo ya Southampton ambayo itakuwa mgeni wa QPR baadaye jioni.

Liverpool vs Everton:
Huu ni mtanange mwingine ambao umeshaanza kuwa gumzo mjini. Liverpool iliyo nafasi ya saba, iliuanza msimu huu kwa kusuasua kutokana na kuonekana kummisi mpachika mabao wao aliyeondoka, Luis Suarez, lakini sasa inaonekana kuanza kuimarika, hasa kutokana na ubora unaoonyeshwa na viungo wawili wa timu hiyo, Raheem Sterling na Philippe Coutinho.
Kwa upande wa Everton wanaonekana kutokuwa sawa msimu huu, kwani wameshindwa kuonyesha makali yao ya msimu uliopita ambapo walikuwa wanapigania kuingia kwenye ‘top 4’.
Everton wapo katika nafasi ya 12 na wanatakiwa washinde ili kujiondoka kwenye hatari yoyote ya kushuka daraja na kujiongezea matumaini ya kutafuta nafasi ndogo waliyonayo ya kushiriki michuano ya Ligi ya Europa, lakini Liverpool bado wanapambana kuingia ndani ya nne bora.
Pambano hili litachezeshwa na mwamuzi Muingereza, Antony Taylor. Katika mechi zake tano zilizopita, Liverpool imeshinda mbili, imetoa sare mbili na kupoteza moja, wakati Everton wameshinda mechi moja tu kati ya michezo yao mitano iliyopita huku mingine wakitoa sare.

Takwimu zinaonyesha kuwa, kwenye mechi tano zilizopita baina ya timu hizo, Liverpool imeshinda mara moja huku matokeo mengine yakibaki kuwa ni sare. Ngoma itakuwa pevu leo na lolote linaweza kutokea.

HIVI NDIVYO ALIVYOPUMZISHWA NTAGWABIRA KOCHA ALIYEFARIKI MWEZI TU BAADA YA KUTAKIWA NA SIMBA



Mchezaji wa zamani na kocha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, Jean Marie Ntagwabira amezikwa juzi katika makaburi ya kijeshi jijini Kigali, Rwanda.
WATOTO WA MAREHEMU WAKITOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO


Mwezi mmoja kabla ya kifo chake, Ntagwabira aliwaniwa na Simba lakini mwisho nafasi yake akaitwaa Goran Kopunovic ambaye pia aliiambia SALEHJEMBE kushitushwa na kifo chake.
NTAGWABIRA WAKATI WA UHAI WAKE.
Mchezaji wa zamani na kocha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, Jean Marie Ntagwabira amezikwa juzi katika makaburi ya kijeshi jijini Kigali, Rwanda.

Ntagwabira ,41, amefariki dunia akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu uliofanya ashindwe kupumua.
Mazishi yake yalihudhuriwa na maofisa mbalimbali wa jeshi pamoja na wanamichezo mbalimbali wakiwemo makocha na wachezaji wa timu ya APR.
Wakati wa mazishi yake, Rais wa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa), Vincent Nzamwita alitoa pole kwa wafiwa, wadau wote wa soka la Rwanda pamoja na familia ya marehemu.
 
WACHEZAJI WA APR
Lakini Shirikisho hilo pia likaahidi kuwasomesha watoto wa marehemu kwa kiwango chote cha elimu watakachofikia.
Ntagwabira ,41, amefariki dunia akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu uliofanya ashindwe kupumua.
Mazishi yake yalihudhuriwa na maofisa mbalimbali wa jeshi pamoja na wanamichezo mbalimbali wakiwemo makocha na wachezaji wa timu ya APR.
 
MAOFISA WA JESHI
Wakati wa mazishi yake, Rais wa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa), Vincent Nzamwita alitoa pole kwa wafiwa, wadau wote wa soka la Rwanda pamoja na familia ya marehemu.
Lakini Shirikisho hilo pia likaahidi kuwasomesha watoto wa marehemu kwa kiwango chote cha elimu watakachofikia.


BUNGE LAKOMALIA TIKETI ZA KIELEKTRONIC


bungemaalum_300_183-734254
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii imeitaka serikali kuangalia upya mfumo mzima wa ukataji tiketi wa kielektroniki kwa mashabiki wa mpira wa miguu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Imetaka serikali kuitisha kikao cha wadau wote yaani benki ya CRDB, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), wamiliki wa viwanja, klabu ili kuupitia upya mkataba na kuang mzima         wa uendeshaji.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Mchinga, Said Mtanda (CCM), alisema hayo bungeni jana wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wake kwa mwaka 2014/2015.

Alisema kamati hiyo ilifanya ziara katika uwanja huo wa Taifa, Januari 19, mwaka huu na kukagua jinsi mashine za ki- elektroniki katika Uwanja wa Taifa kuona jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi.

Alisema wajumbe walijionea jinsi watazamaji wa mchezo wa mpira wa miguu wanavyoingia kwa njia ya kawaida tofauti na maelezo kuwa wanatumia kadi za mfumo wa kielektroniki.

"Aidha, mfumo huo umethibitika kuwa hautumiki na kamati haijaridhishwa na utaratibu wa ukataji tiketi unaotumika sasa na tunaitaka serikali kuitisha kikao cha wadau ili kupitia upya mkataba huo," alisema Mtanda.

Alisema kutokana na kamati kutoridhishwa ni vyema kuangalia mfumo huo ili kuongeza mapato kwani bado kuna wanaonunua tiketi hizo kwenye magari na sehemu nyingine.