Jumanne, 2 Juni 2015

EL MERREIKH WAJIVUA KOMBE LA KAGAME, WASEMA HAWAWEZI KUJA KULITETEA DAR



MABINGWA watetezi wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), El Merreikh ya Khartoum, Sudan imesema haitashiriki kutetea ubingwa wake wa michuano itakayofanyika kuanzia Julai 11 hadi Agosti 2 mwaka huu hapa nchini imefahamika.
Akizungumza na MANDELA MBEGEZE BLOG kutoka Khartoum, Ofisa Habari wa El Merreikh, Babiker Osman, alisema kwamba timu hiyo imeamua kujitoa kwenye mashindano ya Kombe la Kagame ni kutaka kuwekeza nguvu zaidi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Wasudan hao wameingia hatua ya makundi..

Osman alisema kuwa wanasikitika kuacha nafasi ya kutetea ubingwa wao na kuongeza kwamba wanaamini waandaaji wa michuano hiyo, Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) wataelewa sababu zao za kujitoa kwenye michuano hiyo na wako tayari kushiriki kwenye michuano ya mwakani endapo watapata nafasi.

"El Merreikh haitashiriki Kombe la Kagame mwaka huu, sababu kubwa ni kujiandaa na mechi za makundi za mashindano ya Ligi ya Mabingwa, zitakuja timu nyingine kutoka Sudan", alisema Osman.
Alizitaja timu nyingine zitakazokuja kushiriki michuano hiyo kutoka Sudan ni Al Hilal ya Omdurman na Khartoum National ya Khartoum.
Baadhi ya timu nyingine zinazotarajiwa kushiriki mashindano hayo mwaka huu ni pamoja na Azam, Yanga, Simba zote za jijini Dar es Salaam, Gor Mahia (Kenya), KMKM (Zanzibar) na APR ya Rwanda.

El Merreikh ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame mwaka jana jijini Kigali, Rwanda kwa kuwafunga wenyeji APR bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa Amahoro mbele ya Mlezi wa Cecafa na Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame.

Bingwa wa michuano hiyo inayofanyika kila mwaka hupata zawadi ya Dola za Marekani 30,000 wakati mshindi wa pili huondoka na Dola za Marekani 20,000 huku timu itakayomaliza ya tatu itajinyakulia Dola za Marekani 10,000.
Katika mashindano hayo mwaka jana Tanzania Bara iliwakilishwa na Azam baada ya Yanga iliyokuwa chini ya Mbrazil, Marcio Maximo ambayo ilipaswa kushiriki kujitoa.

Jumamosi, 7 Februari 2015

andrew ayue alieipeleka ghana final

hizi ndizo mechi za ligi kuu ya soka ya tz bara wiki hii

TAREHE 7.2.2015

 16:00 POLISI MORO - : - AZAM FC

16:00 NDANDA FC - : - STAND UNITED

16:00 KAGERA SUGAR - : - MGAMBO JKT

16:00 T.PRISONS - : - RUVU SHOOTING
 16:00 JKT RUVU- : - MBEYA CITY

16:00 COASTAL UNION - : - SIMBA SC


 MICHEZO INAYOKUJA

 2015-02-08 16:00 YANGA Vs MTIBWA SUGAR Uwanja wa taifa

RnTimuPWDLFAGdPts
1YANGA12642137622
2Azam FC11632158721
3MTIBWA SUGAR11461137618
4POLISI MORO13463109118
5JKT RUVU135351313018
6RUVU SHOOTING1353599018
7Coastal Union13454109117
8SIMBA SC123721311216
9MBEYA CITY1243588015
10KAGERA SUGAR133641011-115
11MGAMBO SHOOTING11425610-414
12NDANDA FC134271117-614
13STAND UNITED13256816-811
14T. PRISONS12174911-210

MASHART YA KOPUNOVIC KWA BEKI OWINO


Kocha wa Simba, Goran Kopunovic, amempa masharti magumu beki wa timu yake hiyo, Joseph Owino ambaye amerejea uwanjani hivi karibuni baada ya kukaa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama paja.

Owino alianza mazoezi mepesi wiki iliyopita na anatarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake hivi karibuni, hivyo akirudi kikosini kutakuwa na vita kubwa ya namba kati yake na mabeki Hassan Isihaka na Juuko Murshid ambao kwa sasa wapo kwenye kiwango kizuri.
Kopunovic amesema hawezi kumpa nafasi kwa kuwa anahitaji kuangalia kiwango chake na nidhamu kabla ya kumpa nafasi ya kucheza licha ya kuwa Owino alikuwa nahodha wa timu hiyo kabla kocha huyo hajatua klabuni hapo.
“Owino ana nafasi ya kucheza japo mabeki wote wapo katika viwango vizuri, lakini siwezi kusema namhakikishia namba kwa sasa, lazima aonyeshe kiwango.
“Sipendi kumuona beki ambaye katika kila mchezo anapewa kadi au kusababisha penalti, kama hatakuwa na tabia hizo basi ana nafasi kubwa ya kucheza,” alisema Kopunovic.

ILE ISHU YA BUSU KANAVARIO AMUOMBA MSAMAHA YULE ASKARI WA KIKE



Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amemuomba radhi askari aliyemkimbilia na kwenda kumkumbatia dakika chache baada ya kufunga bao katika mechi dhidi ya Coastal Union.

Cannavaro alifunga bao hilo katika dakika ya 11, Jumatano iliyopita na kufanya kitendo hicho ambacho kilikuwa gumzo.
 Cannavaro alisema alimuomba askari huyo msamaha muda mfupi baada ya mechi hiyo ambapo aliamua kumfuata na kumueleza kuwa hakuwa na nia mbaya.
Cannavaro alisema anamshukuru askari huyo kwa kukubali maombi yake ya msamaha aliyoyatoa kwani hakutarajia hali hiyo kutokea kutokana na furaha aliyoipata baada ya kufunga bao hilo.
“Kiukweli nilifanya kosa kukimbia na kwenda kumkumbatia askari wakati nashangilia bao nililolifunga, nilijikuta ghafla nafanya kitendo kile bila kutarajia, sikukitarajia kabisa wala sikupanga iwe hivyo.

“Baada ya mechi kumalizika nilimfuata nikazungumza naye, pia walikuwepo baadhi ya viongozi wangu na wale wa polisi niliwaomba radhi kwa kitendo hicho nilichokifanya, 
nikashukuru wakanielewa na kulimaliza tatizo hilo,” alisema Cannav


TABIA za beki mkongwe wa Chelsea, John Terry, ni kupenda kujitambulisha kwa washambuliaji anaokutana nao wakati timu yake ikiwa uwanjani.
Terry, maarufu kama JT, hajitambulishi kwa kupeana mikono, badala yake maneno ya kibabe au kumgongagonga mshambuliaji anayekuwa anamkaba ili kumuonyesha siku hiyo shughuli ni pevu.

Nahodha huyo wa Chelsea amekuwa akifanya hivyo mara nyingi ikionekana kutaka kumtawala mapema kabisa kisaikolojia mshambuliaji anayemkaba kwamba ajue amekutana na kiboko yake au beki katili na asiyetaka mchezo na kazi yake.
Wakati akiwa Liverpool, mshambuliaji Fernando Torres aliwahi kusema kila walipokutana na Chelsea alifanya juhudi kubwa kuhakikisha anafunga kwa kuwa alitaka kumuonyesha Terry ambaye hakufurahishwa na ubabe wake mara kwa mara.
Huenda mara kadhaa, Terry amekuwa akibadili mbinu zake, lakini hiyo ni moja ya kubwa alizonazo. Wakati fulani, mpango huo wa Terry ulifeli.

Katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, Terry alianza mapema mipango yake ya kutaka kumuonyesha mshambuliaji Diego Costa kwamba yeye ni nani. 
 
Lakini majibu yalikuwa makali kuliko alivyotegemea na ndipo akagundua kuwa Costa ni namba nyingine na huenda mfumo alioutumia kwa mara ya kwanza haukuwa sahihi.
Kitendo cha Costa kuwakanyaga mabeki Emre Can na Martin Skrtel wa Liverpool kimewafanya wengi waamshe mjadala wa mshambuliaji huyo raia wa Hispania mwenye asili ya Brazil.
Maswali yamekuwa ni mengi, kama kweli anafaa kuichezea Chelsea, kama kweli wanastahili kuwa na mchezaji mkatili hivyo. Mwisho wengi wanahoji vipi awe mjeuri namna hiyo? Ingawa wanavutiwa na uwezo wa kazi zake maana ndiye anaongozwa kwa kutikisa nyavu katika Ligi Kuu England.
Costa ni mtoto wa Uswahilini, amekulia maisha hayo na hakuwahi kuishi maisha ya mafunzo ya soccer kwenye ‘academy’ kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Ulaya.
Ubabe wa mechi za mchangani ambazo alikuwa maarufu sana, bado uko kwenye damu yake, ndiyo maana anawapa tabu sana Wazungu.
Costa alizaliwa katika mji mdogo wa Lagarto katika Jimbo la Sergipe nchini Brazil. Miaka yote alikuwa akicheza soka la mchangani na alikuwa maarufu sana.
Hadi alipofikisha miaka 16, ndiyo alichukuliwa hadi jijini Sao Paulo na kujiunga na timu iliyokuwa na mafunzo sahihi ya mchezo wa soka.
 
Waliocheza naye soka katika Mji wa Lagarto kabla hajaondoka kwenda Sao Paulo, wanasema alikuwa mjeuri, mtu mwenye hasira na hakuwa na woga hata kidogo.
Lakini kituko cha kumpiga mchezaji halafu akakimbilia kumsukuma na kumghasi mwamuzi kilikuwa maarufu zaidi. Baadaye Costa alifungiwa miezi minne. Wakati huo alikuwa akiichezea Barcelona Esportiva Capella.
Aliwahi kubatizwa jina la Picardia, neno hilo la Kihispania lenye maana ya mpiganaji au mtu asiye na hofu na ndivyo anavyoonekana.
Hii inaonyesha kiasi gani uchezaji wa kibabe Costa hautakwisha na ataendelea kuwa namna hiyo kwa kuwa hakucheza soka la mafunzo linalomuonyesha afanye vipi kuonekana ni mwenye nidhamu.
Takwimu zinaonyesha hata kabla ya msimu kwisha, ameshasababisha tafrani za kawaida mara 22, amekwidana na mabeki mara tano, amewasukuma kwa kifua mara 13, amewasukuma kwa mikono mara 15 na amekutana na mabeki uso kwa uso na kutoa maneno ya kibabe mara 11.
Pamoja na kwamba ameshakutana na adhabu kutoka FA, lakini haimbadilishi yeye kuwa alivyo na wengi wamekuwa wakisema ni zawadi nzuri kwa mabeki wa England ambao wengi wamekuwa wababe kwa washambuliaji.
 Mara kadhaa, Costa ameonekana akiwa amechaniwa jezi au bukta. Lakini amekuwa akionyesha sehemu alizoumizwa na viatu vyenye njumu za chuma za mabeki hao ambao sasa wameanza kulalamika.
Hakuna ubishi tena unaweza kusema ubabe wa Costa ni dawa ya mabeki wababe wa England na karibu kila mchezo amekuwa akizozana nao na mara nyingi kuwafanya wadau wa soka kuwaonea huruma mabeki.
 
Kwa zaidi ya miaka 20, hakuna aliyewahi kulalamika mabeki wa Ligi Kuu England wamekuwa wakionewa hadi Costa alipotua England. Je, ataendelea hivyo hadi mwisho?
Mabao anayofunga anaonyesha ana uwezo na hilo alilidhihirisha Hispania kabla ya kutua England. Je, kuna mengi anafunga baada ya kuwatisha mabeki?
 
Jiulize, mabeki wa England hasa wale wa kati ambao wengi ni wakatili, wataendelea kumvumilia na kushitaki bila ya kumtafutia dawa?
Ila ukweli, mtoto wa Uswahilini anawapa shughuli mabeki hao licha ya wao kutamba kwamba England ndiyo kwa wababe.
Kwa sasa Costa ni kati ya burudani zinazovutia zaidi katika soka England. Kila anapokuwa anaitumikia Chelsea, wengi hupenda kuona anavyofunga na sasa imegeuka, wengi wanapenda kuona anavyopambana na mabeki wababe.

07 Feb 2015